Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 28.11.2020: Haaland, Tagliafico, Kana, Bettinelli, Vydra

Erling Braut Haaland aliifungia Borussia Dortmundbao la kwanza dhidi ya Bruges katika Champions League
Maelezo ya picha,

Erling Braut Haaland has scored 17 goals in 13 games for Borussia Dortmund this season

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema anatazamia kumuona mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland katika klabu hiyo "kwa muda mrefu". Nyota huyo aliye na miaka 20- ana mkataba na klabu hiyo ya Bundesliga hadi mwaka 2024, lakini anaweza kuondoka kwa euro milioni 75 (£67m) mwaka 2022 kwasababu ana kifungu kinachomruhusu kufanya hivyo katika mkataba wake wa sasa. (Bild Sport - in German)

Klabu za Ligi ya Primia zimeombwa kupunguza idadi ya mashabiki wanaoruhusiwa uwanjani hadi 1,000. Mamlaka ya usalama wa viwanja vya michezo imesema agizo hilo linastahili kuzingatiwa kwa muda hadi pale mashabiki 2000 wataruhusiwa uwanjani. (Telegraph - subscription only)

Winga Muingereza Angel Gomes, 20, anasema aliondoka Manchester United 'kutafuta mwanzo mpya' baada ya kukataa ofa yao na kujiunga na Lille. (Independent)

Maelezo ya picha,

Angel Gomes, 20, anasema aliondoka Manchester United 'kutafuta mwanzo mpya'

Mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Anderlecht Mbelgiji Marco Kana, 18, amesema Liverpool ndio klabu anayotamani kujiunga nayo atakapoamua kuhama. (Walfoot, via Liverpool Echo)

Kipa wa Fulham Marcus Bettinelli, 28, ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia. Kipa huyo ambaye kwa sasa yuko Middlesbrough kwa mkopo, alijumuishwa katika kikosi cha kitaifa cha England na Gareth Southgate mwaka 2018. (Mail)

Mshambuliaji wa Burnley na Jamhuri ya Czech Matej Vydra, 28, anataka kuondoka Turf Moor ili kupata nafasi ya kucheza soka ya kikosi cha kwanza. (Accrington Observer)

Maelezo ya picha,

Matej Vydra(Kulia) amekuwa na Burnley tangu mwaka 2018

Mchambuliaji Muingereza Joe Garner, 32, anaondoka Wigan Athletic kati kati ya msimu baada ya kukubali kuhamia Super League ya India. (Football Insider)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameahidi kuongeza msaada wake wa chakula kwa shirika la watoto na kutoa wito kwa wachezaji zaidi wa soka kumsaidia mshambuliaji wa England na United Marcus Rashford, 23, katika kampeni yake ya kuwakinga watoto dhidi ya njaa. (Times - subscription required)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford anasema kusaidia watoto "ni muhimu sana" wakati wa Janga la corona

Beki wa kushoto na nyuma wa Argentina Nicolas Tagliafico ambaye amehusishwa na Chelsea na Manchester City, amekubali kurefusha mkataba wake na Ajax ambayo unatarajiwa kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kusalia katika klabu hiyo hadi angalau mwisho wa msimu . (De Telegraaf - in Dutch)

Mkurugenzi wa kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini amekiri kuwa anamtaka winga wa Ufaransa Florian Thauvin, 27, ambaye mkataba wake Marseille unakamilika mwaka 2021. (Telefoot, via Football Italia)