Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 23.10.2020: Pochettino, Ozil, Garcia, Malen, Kabak

Mauricio Pochettino anawania nafasi ya Zidane
Maelezo ya picha,

Mauricio Pochettino anawania nafasi ya Zidane

Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino na meneja wa sasa wa timu ya akiba ya Real Madrid Raul wanashindania kukaba nafasi ya timu hiyo kubwa zaidi ya Uhispania iwapo wataamua kumfukuza Zinedine Zidane ambaye anakabiliwa na shinikizo. (AS)

Meneja wa Manchester City Guardiola ana matumaini kuwa anaweza "kumshawishi" mlinzi wa uhispania Eric Garcia, 19, kuongeza mkataba wake. (Independent)

Maelezo ya picha,

Mesut Ozil

Mchezaji wa safu ya kati ya Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil anaweza kuhamia katika klabu ya Marekani ya MLS huku DC United ikionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Sun)

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na Donyell Malen, 21, kutoka klabu ya PSV Eindhoven, miaka mitatu baada ya kumuuza mshambuliaji Muholanzi kwa thamani ya £540,000. (Soccernews, via Star)

Maelezo ya picha,

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na Donyell Malen

Mkataba wa Everton wa kumsaini mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 23, kutoka Sheffield United mwaka 2016 ulikuwa "wa bei ya chini" kuliko ilivyoripotiwa kwamba alisainiwa kwa malipo ya £1.5m, kulingana na meneja wa timu ya Toffees vijana wenye chini ya miaka -23 David Unsworth. (Sky Sports, via Mail)

Tottenham walishusha chini kiwango cha bei ya difenda Wales Joe Rodon, 23, kwa pauni milioni 5 baada ya kukataa kutimiza kiwango kilichotakiwa cha bei cha Swansea kulingana na tarehe ya mwisho ya EFL . (Football Insider)

Maelezo ya picha,

Liverpool wanatafuta mtu wa kuziba pengo la Virgil van Dijk

Liverpool wanaweza kugeuzia nia yao kwa difenda wa Schalke ambaye pia ni difenda kimataifa wa Uturuki Ozan Kabak, 20, huku msako wa kumtafuta mchezaji atakayeziba pengo la safu ya kati-nyuma rililoachwa na Virgil van Dijk, 29, ukiendela. (Sport Media Set, via Sport Witness)

Difenda wa Barcelona kutoka Catalania Gerard Pique, mwenye umri wa miaka 33, alikubali kupunguza malipo yake kwa 50% kwa kipindi kilichosalia cha msimu, kwasababu ya athari za mzozo wa corona. (Sport)

Maelezo ya picha,

Muhamed Besic ataamua msimu ujao ni timu gani atakayohamia

Kiungo wa kati wa Everton ambaye hajachukua maamuzi Mbosnia Muhamed Besic, 28, hata lazimisha kuunga kuhamia Ureno - ambayo ni moja ya timu kubwa za ligi ya ulaya ambazo bado hazijafunga dirisha lake la uhamisho -na atasubiri Januari kuamua ni klabu gani atakayohamia. (Liverpool Echo)

Arsenal wamejaribu kumpa mafunzo mtoto wa kiume wa mshambuliaji wake wa zamani Mholanzi Dennis Bergkamp. Mitchel Bergkamp, 22, amekuwa akifanya mazoezi katika London Colney pamoja na vijana wa Steve Bould wa chini ya miaka 23. (Goal)

Maelezo ya picha,

Sergio Reguilon anasema mourinho alikuwa na nafasi kubwa katika kuhamia kwake Tottenham

Mlinzi wa Uhispania Sergio Reguilon, 23, anasema meneja wa zamani wa Real Madrid Jose Mourinho alikuwa mtu muhimu katika kuhamia kwake Tottenham. (Sky Sports)

Newcastle wametoa ofa ya mkataba hadi mwisho wa msimu huu kwa mshambuliaji Mfaransa Florent Indalecio, mweney umri wa miaka 23. (Newcastle Chronicle)

Maelezo ya picha,

Aaron Wan-Bissaka anataka kupata tena nafasi katika kikosi cha England

Difenda wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka anataka kupata tena nafasi katika kikosi cha England na atakataa kubadilisha nchi kuwakilisha DR Congo. (Telegraph - subscription required)

Kiungo wa kati wa Scotland Darren Fletcher, 36, amerudi katika Manchester United kwa kazi ya muda ya ukocha kusaidia ukuaji wake. (Manchester Evening News)

Maelezo ya picha,

Hakim Ziyech anasema fursa ya kushinda vikombe kwa kucheza "mchezo mzuri" ndio sababu iliyompeleka Stamford Bridge

Kiungo wa kati aliyewasili Chelsea msimu huu Mmorocco Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 27, anasema fursa ya kushinda vikombe kwa kucheza "mchezo mzuri" ilikuwa ni sababu ya yeye kuhamia Stamford Bridge. (London Evening Standard)

Maelezo ya picha,

John McGinn anahisi yuko fiti sasa kuliko awali

Kiungo wa kati wa Aston Villa Mskochi John McGinn, 26, anasema kuwa anahisi yuko fiti baada ya kupata ugumu walipofungua msimu katika Primia Ligi . (Birmingham Mail)

Mashabiki watakuwa tayari kutazama kutazama mechi ya West Ham dhidi ya Manchester City wikendi hii katika katika ukumbi wa sinema uliopo karibu sana na uwanja wa mpila ambao utakua mtupu. (Times - subscription required)