Mzozo wa Tigray Ethiopia: Mji mkuu wa Tigray 'unakabiliwa na mashambulio makali'

Ethiopian soldiers
Maelezo ya picha,

Wanajeshi wanasema wanakaribia kufThe army says it is gaining ground in the northern region of Tigray

Mji mkuu wa jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia unakabiliwa na mashambulio makali ya kutoka kwa vikosi vya serikali, wafanyakazi wa misaada na maafisa wa eneo hilo wanasema.

Eneo la kati kati ya mji wa Mekelle linashambuliwa kwa "makombora," chama tawala katika jimbo la Tigray kinasema.

Jeshi la Ethiopia limekuwa likikabiliana na wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) kwa wiki kadhaa sasa.

Linasema kuwa linatarajia kuchukua udhibiti wa mji huo kutoka mikononi mwa TPLF katika kipindi cha siku chache zijazo , lakini litajizuia kuwadhuru karibu raia 500,000 wanaoishi katika mji huo.

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa, na maelfu ya wengine kutoroka makwao baada ya jeshi la Ethiopia kuteka miji yao.

Awali majeshi ya Ethiopian yalisema kuwa yameteka mji wa Wikro, ulioko kaskazini mwa Mekelle, miongoni mwa miji mingine katika eneo hilo.

Ni vigumu kuthibitisha hali ya vita hivyo kwasababu mfumo wa mawasiliano ya simu na intaneti umekatizwa katika jimbo la Tigray.

Ni nini kinachojiri kwa sasa katika mji mkuu wa Tigray?

Kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael ameambia shirika la habari Reuters kupitia ujumbe wa simu kwama mji wa Mekelle unakabiliwa na "mashambulio makali ya makombora", na kuongeza kuwa vikosi vya serili vimeanza oparesheni ya kuteka mji huo.

Taarifa tofauti kutoka kwa TPLF, iliyoripotiwa na shirika la habari la AFP, inatoa wito kwa "jamii ya kimataifa kulaani mashambulio hayo ya angani kwa kutumia ndege za kivita kutekeleza mauaji".

Pia imelaumu serikali ya Eritrea kwa kuhusika na mashambulio katika mji wa Mekelle.

Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada na wanadiplomasia wameambiwa na wakazi kuwa kwamba walisikia milipuko kaskazini mwa mji huo

Serikali ya Ethiopia haijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulio lake la hivi punde. Siku ya Ijumaa ilisema imeingia kilomita 20 ndani ya mji huo na umeanza "awamu ya mwisho" ya oparesheni yake dhidi ya TPLF.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisemana kuwa vikosi vya taifa "havitashambulia" maeneo yanayokaliwa na raia.

"Usalama wa Waethiopia mjini Mekelle na maeneo mengine katika jimbo la Tigray unaendelea kupewa kipaumbele na serikali kuu," Billene Seyoum aliongeza.

Maelezo ya picha,

Picha hii iliyopigwa kutoka angani inaonesha mji wa Mekelle, ulivyokuwa siku ya Alhamisi

Katika mkutano siku ya Ijumaa, Bwana Abiy aliwaambia wajumbe wa usalama wa Afrika kwamba raia watalindwa.

Hata hivyo, suala la mazungumzo ya amani halikuzungumziwa na wajumbe hao hawakuruhusiwa kuzuru jimbo la Tigray.

Chama cha TPLF, ambacho kinadhibiti mji wa Mekelle, kimeapa kuendelea na mapigano.

Umoja wa Mataifa umeonya uwezekano wa kufanyika kwa uhalifu wa kivita ikiwa majeshi ya Ethiopia yatashambulia Mekelle.

Pia imeelezea hofu yake kuhusu kukosekana kwa njia ya wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kufika eneo hilo.

Siku ya Alhamisi wanajeshi wa Ethiopia walipelekwa katika mpaka wa Tigray na Sudan, kuzuia watu wanaokimbia ghasia kuondoka nchini, kwa mujibu wawakimbizi.

Mwandishi wa BBC Anne Soy , akiwa upande wa mpaka wa Sudan aliona makumi ya wanajeshi wa Ethiopia, katika eneo hilo hali ambayo imepunguza idadi ya watu wanaovuka kuingia Sudan.

Je TPLF ina uwezo gani wa kijeshi?

Ijapokuwa wachanganuzi wanasema kwamba eneo hilo halina uwezo wowote wa kijeshi , imedaiwa kwamba jeshi lake hivi karibuni lilishambulia wanajeshi wa seriikali.

Inakadiriwa kwamba utawala wa Tigray unaweza kumiliki wanajeshi 200,000 ikijumlisha wanajeshi wake na maafisa wa polisi katika eneo hilo.

''Jeshi hilo linashirikisha wanajeshi walioshambuliwa na wenzao wa serikali ya Ethiopia katika siku ya mwisho kwa kuwa lilikuwa jeshi kubwa lilomiliki silaha nyingi'' , alisema jenerali Dolaal Halhal akizungumza na BBC Somali.

Jenrrali huyo anaamini kwamba vita vinavyoendelea katika eneo hilo sio vita haswa. Amesema kwamba wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wamekuwa wakiwasili karibu na jimbo hilo kutoka maeneo mbali mbali ya taifa hilo.

Wengine wanasema kwamba vita hivyo vilianza na kuifanya serikali kuondoa wanajeshi wake kutoka kambi tofauti katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo.

Je wapiganaji wachama cha TPLF wana miliki silaha gani?

Huku wapiganaji hao wakifanikiwa kurusha makombora ya roketi kati miji na viwanja vya ndege nchini Ethiopia pamoja na taifa jirani la Eritrea, kumekuwa na maswali mengi kuhusu silaha zinazomilikiwa na jimbo hilo na zinakotoka.

Alipoulizwa na BBC Somali kuhusu chanzo cha kuwepo kwa silaha zinazotumika na wapiganaji hao, jenerali Dolaal alisema kwamba silaha hizo hazitoki kokote na kwamba tayari zilikuwa katika eneo hilo na zilichukuliwa na wapiganaji wanaounga mkono kujitenga kwa jimbo hilo kupigana na serikali ya Eritrea ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ikikabiliana na Ethiopia.

'Thuluthi moja ya silaha zinazomilikiwa na wapiganaji hao zilisambazwa katika eneo hilo na jeshi la Ethiopia', aliongezea.

Je ni kwnaini Abiy Ahmed alitumia nguvu?

Serikali ya Ethiopia imeshutumu chama tawala cha jimbo la Tigray kukabiliana na wanamgambo katika eneo hilo. Katika hotuba iliorushwa mubashara na runinga alisema kwamba hatua ya kijeshi katika jimbo hilo imefaulu na itaendelea

Taarifa kutoka kwa waziri mkuu Abiy Ahmed ilisema : Wamevuka mpaka na njia ya pekee iliosalia ni kutumia nguvu ili kuokoa raia na taifa.

Ghasia katika eneo hilo zimesababisha wasiwasi katika jimbo la Tigray na sasa wengi wa raia wanaotorokea nchini Sudan pia wanakabiliwa na tisho la maambukizi ya corona.

Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande husika kusitisha mapigano kwa lengo la kuweka amani.