Mohsen Fakhrizadeh: Iran yaapa kulipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi wake

Maelezo ya video,

Students of Iran's Basij paramilitary force rallied in front of the foreign ministry in Tehran

Rais wa Iran ameilaumu Israel kwa mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa ngazi ya juu wa nchi hiyo siku ya Ijumaa, na kukariri kuwa hatua hiyo haitarudisha nyuma mpango wake nyuklia

Hassan Rouhani pia alisema kwamba Iran italipiza kisasi mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh wakati itakapoamua kufanya hivyo.

Fakhrizadeh aliuawa katika shambulio dhidi ya gari lake lililotekelezwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki katika eneo laAbsard, mashariki mwa mji mkuu wa Tehran.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo, lakini iliwahi kumshtumu mwanasayansi huyo kwa kuhusika na mpango wa kisiri wa kuunda silaha za nyuklia.

Mauaji yake huenda yakazua taharuki kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuongeza uhasama kati ya nchi hiyo, Marekani na washirika wake Israel.

Je Iran imepokeleaje mauaji hayo?

Makomanda wa kijeshi wa Iran wameapa kulipiza kisasi mauaji hayo.

"Kwa mara nyigine tena, mikono ya maadui wa ulimwengu waliojawa na kiburi wametuulia mtu wetu," (maneno aliyotumia kuashiria Israel), Rais Hassan Rouhani alisema katika taarifa, kwa mujibu wa televisheni ya kitaifa.

"Mauaji ya shujaa Fakhrizadeh yanaonesha kuwa maadui wetu' walivyotetereka na kiwango chao cha chuki dhidi yetu... Ushujaa wake hautarudisha nyuma mafanikio yetu."

Maelezo ya video,

The road near Tehran where gunmen opened fire on Mohsen Fakhrizadeh

Hossein Dehghan, mshauri wa kijeshi wa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameapa "kuwashambulia" walitekeleza mauaji hayo kama radi.

Iran inasisitiza mpango wake wa nyuklia ni salama na lengo lake ni la amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, amelaani mauaji hayo nakusema kuwa ni "kitendo cha ugaidi wa kitaifa''

Mashirika ya ujasusi ya magharibi yanaamini Fakhrizadeh alikuwa anasimasimamia mpango wa kisiri wa uundaji silaha za nyuklia za Iran.

"Endapo Iran ingeliamua kuunda silaha za nyuklia, Fakhrizadeh angelifahamika kama baba wa mabomu ya Iran," mmoja wa wanadiplomasia wa Magharibi aliambia shirika la habari la Reuters mwaka 2014.

Lakini taarifa ya mauaji hayo zinajiri wakati kumekuwa na hofu mpya kuhusu uzalishaji wa madini ya urani unaofanywa na nchi hiyo.

Madini ya urani ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa kawi ya nyuklia na silaha za kijeshi za nyuklia.

Maelezo ya picha,

Mohsen Fakhrizadeh, alikuwa mkuu wa kitengo cha utafiti na uvumbuzi katika wizara ya ulinzi

Mkataba wa mwaka 2015 uliofikiwa na nchi sita zener uwezo duniani uliweka kiwango cha ukuzaji wa madini hayo, lakini tangu Rais Donald Trump alipojiondo katika mkataba huo mwaka 2018, Iran imekiuka makusudi makubaliano hayo.

Joe Biden amekubali kushauriana upya na Iran atakapoingia rasmi madarakani mwezi Januari kuwa rais wa Marekani, licha ya Israel kupinga hatua hiyo kwa muda mrefu. e longstanding opposition from Israel .

Kati ya mwaka 2010 na 2012, wanasayansi wanne wa nyuklia wa nchi hiyo wameuawa na Iran imelaumu Israel kwa kuhusika na mauaji hayo.

Jina la Fakhrizadeh lilitajwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika maelezo yake kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran mwezi April mwaka 2018.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa za mauaji ya mwanasayansi huyo.Pentagon pia imekataa kutoa kutoa kauli yoyote, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Ni nini kilimkuta Mohsen Fakhrizadeh?

Katika taarifa siku ya Ijumaa, wizara ya ulinzi ya Iran ilisema: "Magaidi waliyojihami walilenga gari lililokuwa limembeba Mohsen Fakhrizadeh, mkuu wa wizara hiyo katika shirika la utafiti na uvumbuzi.

"Baada ya makabiliano kati ya magaidi hao na walinzi wake, Bwana Fakhrizadeh alijeruhiwa vibaya ba kukimbizwa hospitali.

"Kwa bahati mbaya jitihada za madaktari kuokoa maisha yake hazikufabikiwa na muda mfupi baadaye akafariki."

Taarifa za vyombo vya habari nchi Iran zinasema washambuliaji walimiminia risasi gari la mwanasayansi huyo.

Shirika la habari la Fars awali liliripoti kuhusu mlipuko wa gari katika mji wa Absard, huku waliyoshuhudia tukio hilo wakdai kuwa "watu watatu hadi wanne waliyodaiwa kuwa magaidi wakiuawa".

Kwanini alilengwa?

Kama mkuu wa wizara ya ulinzi katika kitengo cha utafiti na uvunmbuzi, Fakhrizadeh bila shaka alikuwa kiungo muhimu. Ndio maana Benjamin Netanyahu alitoa onyo, miaka miwili iliyopita "wakumbuka jina lake".

Tangu Iran ilipoanza kukiuka utekelezaji wa mktaba wa nyuklia uliyofikiwa mwaka 2015, nchi hiyo imeendelea mbele na hatua ya kukuza madini ya urani kuimarisha uzalishaji huo kupita kiwango kilichokubailiwa.

Maafisa wa Iran wamekuwa wakisema hatua kama hizo zinaweza kurudishwa nyuma lakini utafiti na maendeleo ni vigumu kufutilia mbali.

"Hatuwezi kurudi nyuma," Balozi wa zamani wa Iran katika Shirika la Kimataifa la Kawi ya Atomiki (IAEA), Ali Asghar Soltanieh, alisema hivi karibuni.

Ikiwa Mohsen Fakhrizadeh alikuwa kiungo muhimu kama vile Israel inavyodai, basi mauaji yake yanaashiria jaribio la kupunguza kasi ya Iran kuendelea mbele na mpango wake wa nyuklia.

Huku rais mteule wa Marekani, Joe Biden, akizungumzia mpangio wa kurudisha Washington katika mkataba wa nyuklia wa Iran, mauaji ya mwanasayansi huyo huenda yalilenga kusambaratisha majadiliano yoyote ya siku zijazo kuhusu suala hilo.

Mohsen Fakhrizadeh ni nani?

Fakhrizadeh alikuwa mwanasayansi mashuhuri wa masuala ya nyuklia na afisa wa ngazi ya juu wa kikosi maalum cha jeshi la Iran.

Ametajwa kwa muda mrefu na vyanzo vya usalama katika nchi za magharibu kuwa na uwezo mkubwa na kiungo muhimu katika mpango wa nyuklia wa Iran.

Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na Israel mwaka 2018, aliongoza mpango wa kutengeza silaha za nyuklia.

Wakati huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, alisema alimtambua Fakhrizedeh kama mwanasayansi katika mpango huo, na kutoa wito kwa watu "kukumbuka jina hilo".

Mwaka 2015, gazeti la New York Times lilimlinganisha na J Robber Oppenheimer, mwanafizikia aliyeongoza mradi wa nyuklia wa Manhattan uliochangia kuundwa kwa silaha za atomiki wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Fakhrizadeh ni profesa wa fizikia ambaye amesemekana kuongoza mradi wa Amad, ambao ni mradi wa kisiri uliobuniwa mwaka 1989 kufanya utafiti wa uwezekano wa kuunda bomu nyuklia. Mradi huo ulifungwa mwaka 2003, kwa mujibu wa IAEA, japo kuwa Bwana Netanyahu alisema nyaraka zilizopatikana mwaka 2018 zilionesha Fakhrizadeh aliendelea kuongoza kisiri mradi huo wa Amad.

Kwa muda mrefu IAEA imetaka kuzungumza naye kama sehemu ya uchunguzi wa mpango wa nyuklia wa Iran.

Hofu ya kwamba Irana inatumia mpango huo kama kisingizio cha kuunda bomu la nyukilia lilifanya Muungano wa Ulaya EU, Marekani na Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwa nchi hiyo mwaka 2010.