Vurugu Nigeria: Mashuhuda wa mauaji Nigeria wadai ‘polisi waliwapiga risasi’

Watu kadhaa wameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa ama kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga ukatili wa polisi mjini Lagos.

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC ilionekana 'kama vita' na kuongeza kwamba maandamano hayo yalikuwa ya amani lakini wanajeshi waliwapiga risasi kwa lengo la kuwaua.

Jeshi la Nigeria limekana kuhusika na mauaji hayo. Mashuhuda waliozungumza na BBC hawakujitambulisha kwa kuhofia usalama wao.