Je ripoti ya BBI ndio suluhisho la amani na umoja wa kudumu Kenya

Ripoti kuhusu mchakato rasmi wa kuleta maridhiano ya kitafa nchini Kenya almaarufu BBI, iliyowasilishwa jana kwa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi mkuu wa Upinzani Raila Odinga inazidi kuibua maoni mseto miongoni mwa wakenya.

Ripoti hiyo iwapo itapitishwa italeta mabadiliko makubwa katika mfumo wa uongozi wa kitaifa, kwa mfano kurejesha wadhifa wa waziri mkuu na kuondolea mbali wadhifa wa wawakilishi wa wanawake bungeni.

Wanaoiunga mkono Ripoti hiyo wanainadi kama muongozo wa kuleta amani na umoja wa kudumu nchini Kenya, usiojikita kwa siasa za kikabila na mivutano ya viongozi. Hiyo itawezekanaje? Mwandishiwa BBC Caro Robi amezungumza na Paul Mwangi, katibu wa jopo hilo la BBI.