Safa na Marwa: Mapacha waliotenganishwa vichwa waruhusiwa kwenda nyumbani

Watoto mapacha wasichana waliozaliwa wakiwa vichwa vyao vimeshikanana na kutenganishwa mwaka jana katika hospitali moja huko London wamerejea nyumbani nchini Pakistan.

Safa na Marwa Bibi walifanyia upasuaji mkubwa mara tatu, na uliochukua zaidi ya saa 50 katika chumba cha upasuaji.

Mama yao, Zainab Bibi, ameiambia BBC ni furaha yake kwamba umefika wakati wa kuwapeleka watoto hao nyumbani kuendelea na maisha yao kama kawaida.