Jurgen Klopp asema Everton ndio itakayomtoa jasho ligi kuu ya premia msimu huu

Klopp na Ancelloti

Meneja wa Everton Carlo Ancelotti anaweza kmwa mshindani mkuu wa Liverpool katika ligi ya premia kulingana na mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp.

Everton inaongoza katika jedwali la ligi ikiwa imeshinda mara nne katika mechi nne chini ya usimamizi wa raia huyo wa Itali ambaye aliajiriwa Disemba iliopita.

Wanacheza dhidi ya mabingwa Liverpool nyumbani Merseyside siku ya Jumamosi.

''Kile ninachofikiria kuhusu Carlo Ancelloti hakikuwa siri . Sikuweza kumuheshimu zaidi . Ni mtu mzuri'' , Klopp aliambia BBC.

''Niliposikia kwamba atakuwa meneja mpya wa Everton , nilijua ushindani mkali mwengine umewasili Uingereza''.

''Walifanya biashara nzuri ya kununua wachezaji wakati wa dirisha la uhamisho la msimu uliopita. Walipata wachezaji waliowahitaji kuimarisha kikosi ambacho tayari kilikua kizuri''.

''Pamoja sasa ni kuzoea kile ambacho Anataka wafanye - kuwafanya kuwa bora zaidi''.

Ancelloti alimrithi Marco Silva kama mkufunzi wa Everton, baada ya kushinda mataji ya ligi akiwa Itali, Ujerumani, Ufaransa na England akiifunza Chelsea 2009-10.

Pia ameshinda mataji matatu ya ligi ya klabu bingwa Ulaya .Everton ambayo ilimaliza katika nafasi ya 12 katika ligi ya Premia msimu uliopita hawajamaliza chini ya nafasi ya saba tangu 2013 -14.

Baada ya kuimarisha safu ya kati katika dirisha la uhamisho la msimu uliopita baada ya kuwasajili wachezaji kama James Rodriguez, Allan na Abdoulaye Doucoure, wana matokeo ya asilimia 100% kutoka katika mechi saba katika mashindano yote msimu huu.

Wamefunga magoli 24 , mshambuliaji mpya wa England Dominc Calvert Lewin akifunga magoli tisa ikiwemo hatrick 2.

Klopp alisema: Calvert Lewin , Nilitaraji kwamba atapiga hatua kubwa katika miaka michache ijayo na amefanya hivyo, alisema Klopp.

''Ana kila unachohitaji kutoka kwa mshambuliaji , kimo, uwezo, malengo, kasi, mzuri angani anapofunga kwa kutumia kichwa na kumaliza na miguu yote''.

''Na sasa timu ina wachezaji bora - wingi zote mbili zina wachezaji huku James na Richarlison. Katika safu ya kati , Allan na yoyote anayecheza pale iwe Sigurdson ama yeyote yule''.

''Kwa kweli ni timu nzuri sana na safu ya ulinzi inafanya kazi yake vizuri kwasababu katika timu nzuri ni rahisi kujilinda nyuma''.

''Hicho ndio unachoona unapoitazama Everton hivyobasi itakuwa mechi ya kufana''.