Wiki ya Afrika kwa picha: 11 - 17 Septemba 2020

Mkusanyiko wa picha bora za wiki kutoka maeneo tofauti barani Afrika:

Maelezo ya picha,

Viongozi wa Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibu Ecowas wakiongoza mazungumzo ya kukwamua mzozo wa kisiasa na wanajeshi wa Mali siku ya Jumanne, katika juhudi za kubuni serikali ya mpito ya kiraia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliyopita.

Maelezo ya picha,

Mafuriko makubwa yanaonekana kuathiri maeneo mengi ya mji mkuu wa Sudan Khatoum katik apicha iliyopigwa kutoka angani siku ya Jumatatu.

Maelezo ya picha,

Mwanafunzi anayeonekana kuwa na usingizi anapiga miyayo siku ya Jumanne wakati Tunisia ilipofungua shule kwa mara ya kwanza tangu ilipoondoa amri ya kutotoka nje iliyowekwa kukabiliana na janga la virusi vya corona mwezi Machi.

Maelezo ya picha,

Siku ya Jumapili wanariadha wa Kenya Hyvin Kiyeng, Mercy Chepkurui na Beatrice Chepkoech -walishindana katika mbio za Istaf nchini Ujerumani.

Maelezo ya picha,

Wanume watatu wakijivinjari majini kwa kutumia mitumbwi mapema asubuhi ya jumanne katika bwawa la Emmarencia mjini Johannesburg, Afrika Kusini...

Maelezo ya picha,

Siku kadhaa zilizopita mkazi wa Soweto, alionekana akitoka saluni...

Maelezo ya picha,

Wengine walionekana hapa nje, pia siku ya Ijumaa.

Maelezo ya picha,

Siku ya Jumatatu maelfu ya wafuasi wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Henri Konan Bédié walihudhuria mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa nchi hiyo. Kiongozi huyo anawania tena kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao. Hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu Alassane Ouattara ana gombea muhula wa tatu madarakani kufuatia kifo cha ghafla cha mshirika wake wa karibu ambaye alitarajiwa kuwa mrithi wake Amadou Gon Coulibaly.

Maelezo ya picha,

Na hapa Wafrika Kusini wanasubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanaharakati aliyepambana na ubaguzi wa rangi George Bizos. Wakili huyo wa haki za binadamu, alimwakilisha Nelson Mandela katika kesi ya Rivonia , alifariki wiki iliyopita akiwa na miaka 92.

Picha zote zina haki miliki kutoka kwa Reuters, EPA na AFP.