Kwanini mpiganaji huyu mzaliwa wa Somalia anatuzwa Italia?

Giorgio Marincola in around 1940

Katika msururu wa taarifa kutoka kwa wanahabari wa Afrika, Ismail Einashe anaangazia jinsi baadhi ya raia wa Italia wanatathmini upya mienendo ya nchi hiyo enzi za ukoloni Afrika.

Baraza la jiji la Rome nchini Italia limepiga kura mapema mwezi huu kuidhinisha kituo kijacho cha treni katika jiji hilo kuu kupewa jina la Giorgio Marincola, Mtaliano mwenye asili ya Kisomali ambaye alikuwa mwanaharakati wa kupigania mageuzi.

Aliuawa akiwa na miaka 21 na vikosi vya Nazi vilivyokuwa vinatoroka katoka kituo cha ukaguzi wa barabarani mnamo Mei 1945, siku mbili baada ya Ujerumani kijisalimisha rasmi kwa Italia mwisho wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia.

Kituo hicho ambacho kwa sasa kinajengwa kilikuwa kipatiwe jina la Amba Aradam-Ipponio - likiashiria kampeini ya Italia nchini Ethiopia mwaka 1936 wakati vikosi vyake vilipotumia silaha za kemikali na kukiri kufanya uhalifu wa kivita katika mapigano ya Amba Aradam.

Maelezo ya picha,

Mchoro unaoonesha vita vya Amba Aradam ambapo gesi ya haradali ilitumiwa

Jina hilo lilibadilishwa baada ya kampeini kuzinduliwa mwezi Juni wakati wa maandamano ya Black Lives Matter kote duniani kufuatia mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd yaliyofanywa na polisi nchini Marekani.

Kampeini hiyo ilianzishwa na mwanahabari Massimiliano Coccia, akisaidiwa na wanaharakati wa vugu vugu la Black Lives Matter, wanahabari wengine na mwandishi Mtaliano mwenye asili ya Kisomali Igiabo Scege na mtoto wa dada yake Marincola, aliyeandika kitabu cha Antar Marincola.

Watu 'weusi wasiogemea upande wowote'

Wanaharakaiti hao kwanza waliweka ubao uliokuwa na ujumbe kwamba kituo hicho kisipatiwe jina la "mnyanyasaji" na kushinikza jina la Marincola, ni fupi lakini mwenyewe atakumbukwa maishani kutokana na juhudi zake.

Maelezo ya picha,

Giorgio Marincola aliondoka kwa mama yake akiwa mdogo na kulelewa na familia yake ya Italia

Alikuwa anafahamika kama "partigiano nero" ama "mweusi asiyeegemea upande wowote" na alikua mwanachama wa vugu vugu la kutetea mageuzi.

1953 alipewa tuzo ya juu katika jeshi la Italia, Medaglia d'Oro al Valor Militare, kutambua juhudi zake.

Marincola alizaliwa 1923 katika eneo la Mahaday, mji uliopo karibu na Mto Shebelle, kaskazini mwa Mogadishu, mji ambao zamani ulitambuliwa kama Somaliland ya Italia.

Mama yake, Ashkiro Hassan, alikua Msomali na baba yake Mtaliano aliyehudumu katika jeshi la Italia akiitwa Giuseppe Marincola.

Maelezo ya picha,

Giuseppe Marincola (kushoto) alitambua kizazi chake cha Somalia

Wakati huo wakoloni wachache wa Italia waliwatambua watoto waliozaliwa kutokana na uhusiano wao na wanawake wa kisomali.

Lakini Giuseppe Marincola iliunga mkono wazo hilo na baadae kuwachukuwa mtoto wake wa kiume na wa kike Isabella, na kuwapeleka Italia kulelewa na familia yake.

Isabella alikuwa muigizaji mkuu wa kike, na moja ya filamu aliyoigiza ni ya Riso Amaro (Bitter Rice), iliyotolewa 1949.

Giorgio Marincola pia alifaulu katika masomo yake ya shule ya upili mjini Rome na hatimaye kujiunga na chuo cha mafunzo ya udaktari.

Wakati wa masomo yake alivutiwa na falsafa ya kupinga ubaguzi. Ndipo alipojiunga na vuguvugu la kupigania mageuzi mwaka 1943 - wakati huo taifa lake la kuzaliwa lilikuwa chini ya utawala wa Italia.

Alijidhihirisha ushujaa wake vitani, kutokana na jinsi alivyotumia ujuzi kuvamia ngome ya maadui na kuwajeruhi. Hata hivyo alishikwa na SS, ambao walimtaka apinge msimamo wa weusi wasioegemea upande wowote katika kituo chao cha redio. Alipokuwa hewani aliripotiwa kukaidi agizo lao, na kusema:

"Nyumbani kunamaanisha uhuru na haki kwa watu wote duniani. Hii ndio sababu napinga ukandamizaji."

Matangazo hayo yalikatizwa na sauti ya jinsi alivyopigwa ilisikika.

'Juhudi za pamoja'

Lakini wanaharakati wanaopinga ubaguzi wa rangi wanataka juhudi zaidi ziongezwe sio tu kubadili jina la kituo cha treni kuwa Marincola, bali wanataka jina hilo liwe mwanga wa kuangazia historia ya ukoloni wa Italia.

Maelezo ya picha,

Sanamu ya mwanahabari Indro Montanelli, aliyetetea ukoloni na kuoa msichana wa Eritrea, 12, iliharibiwa

Wanataka mamlaka mjini Rome kuendelea mbele na kuondoa sanamu zinazotukuza ukoloni katika mji huo.

Uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja mjini Milan, wakati wa maandamano ya Black Lives Matter, ambapo sanamu ya mwanahabari mwenye utata Indro Montanelli, aliyeshinda ukoloni na kukiri kumuoa msichana wa miaka 12 kutoka Eritrea wakati akihudumu jeshini miaka ya 1930 iliharibiwa.

Historia ya Ukoloni wa Italia Afrika Mashariki:

  • 1890: Ufalme wa Italia uliteka Eritrea na kutangaza kuwa koloni lake
  • 1895: Italia ilivamia Ethiopia, na kuibadilisha jina kuwa Abyssinia
  • 1896: Vikosi vya Italia vilishindwa na Waethiopia katika eneo la Adwa - na kutia saini mkataba wa kuitambua kama taifa huru
  • 1889: Italia ilikita kambi kati kati ya Somalia
  • 1935: Wapiganaji wa Italia waliiovamia Ethiopia, walilaumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kivita na kutumia silaha za sumu wakati wa vita
  • 1936: Wataliano waliteka miji ya Addis Ababa. Ethiopia, Eritrea na Somaliland ya Italia na kuzifanya Afrika Mashariki ya Italia
  • 1937: Vikosi vya Italia mjini Addis Ababa viliwaua karibu watu 19,000 ndani ya siku tatu kufuatia jaribio la mauaji dhidi ya mwanamume aliyetuliwa na Mussolini kuongoza koloni hilo
  • 1941: Vikosi vya Uingereza na vya Jumuiya ya Madola vikishirikiana wenyeji vilifanikiwa kuwafurusha Wataliano kutoka eneo hilo

Chakula cha Wasomali

Mwezi uliopita, Somalia ilisherehekea mwaka wa 60 wa uhuru wake.

Kutokana na mzozo wa ndani uliodumu kwa miaka 30 kumbukumbu zote za zama za ukoloni zimetoweka - isipokuwa jikoni ambako chakula asilia cha Wasomali "suugo suqaar"- mchuzi unaotoelwa na "baasto" ama pasta.

Maelezo ya picha,

Chakula cha Wasomali cha "suugo suqaar"na"baasto" kilichoandaliwa na Ismail Einashe, Palermo ilijitokeza kwamba ni maarufu

Wasomali pia waliacha nyayo zao nchini Italia- sio tu kupitia mandugu wa Marincola - bali pia katika uandishi wa vitabu .

Hadi wa leo Wasomali wanachangia idadi kubwa ya wahamiaji wa zamani na wa sasa.

Wale ambao ni wageni Italia wanawaita wenzao waliohamia huko kitambo kama jamii ya "mezze-lira" - kumaanisha "nusu lira" kuashiria utambulisho wao wa nusu Msomali- Mtaliano.

Hatua ya kuitta kituo hicho cha treni Marincola ni muhimu kwa jamii ya Wasomali - kwani inazua kumbukumbu ya kwa Wataliano wote kuhusu ushirikiano wa muda mrefu kati ya Itali na Somalia.