Virusi vya corona : Zifahamu ‘aina’ 6 za covid-19 zenye madhara tofauti na jinsi unavyoweza kuokoa maisha yako kwa kuzitambua

Una enfermera verifica los síntomas de una mujer en México
Maelezo ya picha,

los datos recopilados por los investigadores, las personas pueden experimentar una amplia gama de síntomas diferentes.

Uchambuzi wa watafiti katika chuo cha King's College mjini London nchini Uingereza umeweza kuigawanya Covid-19 katika "aina " sita, kila aina ikitengwa kulingana na upekee wa dalili zake.

Kila moja ya aina hii inaonyesha utofauti katika makali ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona na haja ya kutumia vifaa vya usaidizi wa kupumua wakati mgonjwa anapolazwa ,kwa mujibu wa wanasayansi.

"Matokeo haya ya utafiti yanamaana kubwa katika utoaji huduma na ufuatiliaji wa watu ambao wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuugua zaidi kutokana na covid-19," anasema mwandishi wa utafiti Dkt Claire Steves wa King's College London.

Maelezo ya video,

Virusi vya corona:Shule zinafunguliwa duniani kote, Je watoto watakuwa salama?

Watafiti walioongozwa na Steves walitegemea ukusanyaji wa data zilizokusanywa kutoka katika utafiti wa App ya COVID Sympston, ambayo huwawezesha watumiaji kuipakua na kuingia kupata taarifa kuhusu virusi vya corona.

Ingawa kikohozi kisichokoma, homa na kukosa uwezo wa kutambua harufu kwa ujumla zinatambuliwa kama dalili kuu tatu za covid -19, data zilizokusanywa kutoka kwa watumiaji zinaonyesha kuwa watu wanaweza kupata uzoefu wa dalili tofauti , ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa kinachouma upande mmoja, maumivu ya misuli, uchovu, kuwa na mkanganyiko, kuhara, ukosefu wa hamu ya kula chakula, matatizo ya kupumua, miongoni mwa dalili nyingine.

Kuongezeka kwa ugonjwa pamoja na athari zake, pia hutofautiana kwa kiwango kikubwa baina ya watu, ambapo unaweza kuanzia dalili kama ya mafua ya kawaida hadi mtu kuwa na hali mbaya na hata kifo.

Maelezo ya picha,

Los investigadores basaron sus hallazgos en información de la aplicación COVID Sympston Study App.

Ili kubaini ikiwa dalili za aina fulani huwa zinajitokeza kwa pamoja na jinsi zinavyohusiana na kukua kwa ugonjwa, timu ya wanasayansi ilitumia mashine ya algorithm kuchambua data kutoka katika kundi dogo la watu wapatao 1,600 waliothibitishwa kuwa ni watumiaji wa mashine hiyo, katika nchi za Uingereza na Marekani wanaougua covid-19 ambao walikua wakisajili dalili zao katika mfumo huo kati ya mwezi Machi na Aprili.

Walitegemea kanzidata huru za watumiaji 1,000 nchini Uingereza, Marekani na Sweden waliosajili dalili zao mwezi Mei.

Tathmini ilibaini kuwa makundi sita ya dalili ambayo yalijitokeza kwa nyakati fulani wakati wa kukua kwa ugonjwa yaliwakilisha ''aina'' sita tofauti za Covid-19

Makundi 6 ya dalili za corona

1. "Mafua" Bila homa: Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, maumivu ya misuli, kikohozi, kuvimba kooni, maumivu ya kifua, bila homa.

2. "Mafua" yenye homa : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane ) ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, kikohozi, kuvimba kooni, kupoteza sauti, homa, kukosa hamu ya chakula.

3. Maumivu ya tumbo : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , ukosefu wa hamu ya chakula, kuharisha, kuvimba kooni , maumifu ya kifua na kikohozi.

4.Uchovu wa mwili wa hali ya juu : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua na uchovu wa mwili .

5.Mkanganyiko wa kiwango cha pili : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane), ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua na uchovu wa mwili.

6.Kiwango cha tatu cha kuugua, maumivu ya tumbo na mfumo wa kupumua : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migraine), ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, ukosefu wa hamu ya chakula, kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua, uchovu, maumivu ya misuli, kushindwa kupumua vyema, kuharisha, maumivu ya tumbo.

Wale wote walioripoti dalili waliugua kichwa upande mmoja(migrane) na kupoteza uwezo wa kutambua harufu, na jumla ya dalili nyingine tofauti za ziada kwa nyakati fofauti.

Baadhi ya dalili hizi, kama vile kuwa na mkanganyiko, maumivu ya tumbo, kushindwa kupumua vyema, hazijafahamika bado kama dalili za covid-19.

Hatahivyo zinatofautiana na zile anazopata mgonjwa mahututi.

Wanasayansi tena walifanya uchunguzi juu ya ikiwa watu wanaopata aina fulani ya dalili walikua na uwezekano zaidi wa kuhitaji usaidizi wa kupumua au kuongezewa hewa ya oksijeni.

Walibaini kuwa asilimia ndogo sana ya watu walikuwa katika makundi ya 1, 2, na 3 walihitaji usaidizi wa kupumua; baina ya 1.5% na 3.3%.

Lakini asilimia ya wale waliokuwa na dalili za makundi ya 3, 4 na 5 walikua uwezekano wa kuhitaji usaidizi wa kupumua kwa 8.6%, 9.9% na 19.8%, kila kundi

Zaidi ya hayo, takriban nusu ya wagonjwa katika kundi la 6 waliishia kulazwa hospitalini , wakilinganishwa na asilimia 16% waliokua katika kundi la 1.

Kwa ujumla, wagonjwa wote walioripoti dalili kutoka makundi ya mwisho matatu walionekana kuwa wadhaifu, wakiwa na uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia, na walikua na magonjwa ya kudumu kama vile ugonjwa kisukari, au ugonjwa wa mapafu kuliko wale waliokuwa katika makundi ya 1, 2, na la 3 1 .

Kwa kukusanya taarifa kuhusu dalili siku tano tu baadae baada ya mtu kupata ugonjwa na kujumuishwa na umri, jinsia, uzito wa mwili, na matatizo ya kiafya ya wagonjwa , kikosi cha wanasayansi wa King's College walitengeneza njia inayowawezesha kutambua makundi waliyomo wagonjwa na hatari zao za kulazwa na huduma ya kupumua wanayoweza kuhitaji.

Kwasababu wengi miongoni mwa watu wanaohitaji huduma ya usaidizi wa kupumua huwa wanalazwa hospitalini kwa takriban siku 13 baada ya dalili za kwanza kujitokeza, siku hizo nane za mwanzo huashiria '' tahadhari ya awali '' juu ya ni nani atahitaji kuhudumiwa zaidi.

"Kama unaweza kubashiri ni watu gani watakua katika siku ya tano, unaweza kuwa na muda wa kuwapatia usaidizi na kuwahudumia mapema kama vile kufuatilia kiwango cha oksijeni na viwango vya sukari mwilini, pamoja na kuhakikisha kwamba wana maji ya kutosha mwilini ,"anaeleza Dkt Steves.

"Hizo ni huduma ambazo zinaweza kutolewa nyumbani, kuepuka mtu kulazwa na kuokoa maisha ," alisema..