Trump: 'Somali hakuna serikali, hakuna usalama wala polisi, ni machafuko tu'

Ilhan Omar with the backdrop of the US and Somali flags

Katika msururu wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa Afrika, Ismael Einashe anaangazia jinsi Somalia ilivyojipata katikati ya kampeni za uchaguzi wa Marekani.

Rais Donald Trump anataka kumtumia mbunge Mmarekani mwenye mizizi yake Somalia Ilhan Omar kama ajenda ya kampeni yake ya uchaguzi wa Novemba mbali na taifa lake alilozaliwa.

Katika matamshi aliotoa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Tulsa, Oklahoma, alimshambulia mbunge huyo mwenye umri wa miaka 37 akidai kwamba anataka kuleta machafuko ya Somalia nchini Marekani.

''Anataka kuifanya serikali yetu kuwa kama taifa la Somali analotoka. Hakuna serikali, hakuna usalama hakuna polisi, hakuna chochote ni machafuko tu. Na sasa anatufunza jinsi ya kutawala. Hapana asante''.

Bi Omar ,ambaye aliwasili nchini Marekani akiwa mtoto kama mkimbizi 1995, ni mbunge anayewakilishi eneo la Minnesota, ambalo linashirikisha eneo la Minneapolis ambapo Mmarekani mweusi George Floyd aliuawa na Polisi mwezi Mei, na hivyo basi kuwasha moto wa maandamano ya Black Lives Matter.

Lakini ni taifa analotoka Bi Omar ndilo ambalo bwana Trump alichagua kulishambuliwa akiwa Tulsa, pengine ili kuwafanya watu kusahau changamoto zinazomkabili nyumbani.

Akijibu Bi Omar alisema matamshi yake ni ya 'kibaguzi'. Aliongezea kwamba hasira yake inatokana na kwamba katika kura ya maoni ya hivi karibuni amekuwa nyuma ya mpinzani wake mkuu kutoka chama cha Democrats Joe Biden, katika jimbo lake ambalo ni nyumbani kwa jamii kubwa ya Wasomali Wamarekani.

Children play with the wreckage of a US Black Hawk helicopter in Mogadishu, Somalia in December 1993
Getty
Perhaps the view of Somalia for Mr Trump and his supporters is still tarnished by events in 1993... when US troops launched a disastrous raid in the Somali capital"
Ismail Einashe
Journalist

Rais huyo alimtaja Bi Omar kama mtu aliyejaa chuki, akionya kwamba atakuwa na jukumu la kuchagiza taifa hilo iwapo bwana Biden ataibuka mshindi. Hii ni kinyume na kwamba wawili hao wamekuwa na maoni tofauti katika chama cha Democrat, huku Omar akimuunga mkono mpinzani wa Joe Biden, Bernie Sanders kushinda tiketi ya chama cha Democrat.

Lakini matamshi kama hayo yanamsaidia sana na kwamba ajenda ya kampeni yake katika jimbo hilo imeanza huku Bi Omar na Somalia wakitumika kama ajenda kuu ya kampeni yake.

Ukweli ni kwamba matamshi kama hayo yalitumika mwaka uliopita katika mkutano wa kampeni wa bwana Trump katika jimbo la North Carolina ambapo wafuasi wa Trump waliimba kuhusu Bi Omar: ''Mrudishe kwao! Mrudishe kwao!''

Matamshi hayo yanafanana na yale yaliokuwa yakitolewa na wafuasi wake ya ''Mfungie'' yaliotumika dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton kabla ya uchaguzi wa urais wa 2016.

Bi Omar ambaye ni mkosoaji mkuu wa rais Trump aliiingia mashakani wakati huo - akilaumiwa na wabunge wa Democrat na Republican kwa kueneza chuki dhidi ya Wayahudi na akalazimika kuomba msamaha kwa machapisho ya twitter akidai kwamba wabunge wa Marekani wanaunga mkono Israel kwasababu ya fedha wanazopata kuwashawishi.

Seneta wa Republican Rand Paul alijitolea kununua tiketi ya ndege kwa mtu 'asieshukuru' kama Bi Omar kwenda Somalia. Alipendekeza kwamba anafaa kurudishwa kwao ili kuheshimu Marekani.

Aliekuwa mwanachama wa Republican anaiongoza Somalia

Inaonekana mafikra ya bwana Trump kuhusu Somalia yanatokana na baada ya kupinduliwa kwa Siad Baarre mwaka 1991, ambapo taifa hilo lilichukuliwa kama mojawapo ya mataifa yaliofeli duniani.

Maelezo ya picha,

Mohamed Abdullahi Mohamed alibadilisha uraia wake Marekani kuwa Rais wa Somalia

Hii inamshirikisha rais wa sasa Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu Farmajo ambaye alisajiliwa kama mwanachama wa Republican katika eneo la Buffalo na kuwachilia uraia wake wa Marekani ili kupigania urais 2017.

Mbali na hayo kuna jamhuri ya Somaliland iliojiondoa na ambayo imefanikiwa kufanya uchaguzi ulio huru na hata iwapo sio taifa linalotambuliwa, ndio eneo lililochaguliwa kidemokrasia ikilinganishwa na mengine katika upembe wa kaskazini mwa Afrika.

Pengine fikra za bwana Trump na wafuasi wake bado zimechafuliwa na matukio ya 1993 - mojawapo ya uvamizi wa Marekani barani Afrika, wakati wanajeshi wa Marekani walipovamia mji mkuu wa Somalia Mogadishi na kumkamata mbabe wa kivita aliyekuwa na uwezo mkubwa.

Ndedge mbili aina ya black Hawk ziliangushwa, huku wanajeshi 18 wa Marekani na zaidi ya raia 500 wa Somalia wakiuawa katika vita hivyo.

Picha za wanajeshi wa Marekani wakiburuzwa katika barabara kuu ziliwashangaza raia wa Marekani na iliathiri pakubwa sera ya kigeni ya Marekani katika eneo hilo.

Maelezo ya picha,

Kuna baadhi ya maeneo nchini Somalia ambako maisha yanaendelea kama kawaida

Lakini chini ya uongozi wa rais Trump, Marekani imekuwa katika vita vya kisiri nchini Somali dhidi ya kundi la wapiganaji wa al-shabab kwa kutumia ndege zisizo na rubani na vikosi maalum, kitu ambacho ni Wamarekani wachache wanachofahamu.

Baadhi ya raia wa Somali wanachukulia mtazamo wa rais Trump dhidi ya taifa lao kuwa wa kutatanisha, wakidai kwamba ni kutokana na sera zake za kigeni ndiposa taifa hilo limekuwa hatari zaidi - na kusema raia wa Somalia na sio wapiganaji wamekuwa wakiuawa kutokana na mashambulizi ya ndege zisio na rubani ambayo yameongezeka chini ya uongozi wake.

Mwanamke Muislamu anayejivunia kuvaa Hijab

Kuanguka kwa Somalia, karibia miongo mitatu iliopita, kuliwatawanya Wasomali duniani kutoka Arctic hadi New Zealand.

Nchini Marekani, mjini Mineapolis ni nyumbani kwa idadi kubwa ya raia wa Somali wanaoishi katika taifa la kigeni duniani - jamii ya watu weusi ambayo ni ya dini ya kiislamu.

Tangu shambulio la bomu la 9/11 kumekuwa na mjadala mbaya dhidi ya Waislamu nchini Marekani. Bwana Trump mara kwa mara hutumia matamshi dhidi ya Waislamu akionesha mfano wa ''wahamiaji wazuri dhidi ya wabaya'', na kuzidisha hofu iliopo.

Maelezo ya picha,

Ilhan Omar alihamia Minneapolis, ambako kuna idadi kubwa ya wakaazi kutoka ya Wasomali, akiwa mdogo

Kwa Trump, bi Omar sio 'muhamiaji mzuri'. Mwanasiasa huyo anayejivunia kuvalia Hijab alipigania haki yake kuvalia vazi hilo bungeni , hatua iliobadilisha sheria ya takriban miaka 181 iliokuwa imepigwa marufu

Haogopi kuwa Muislamu - kitu ambacho kinamtofautisha yeye na mwanamke mwengine mwenye mizizi ya Kisomalia Ayaan Hirsi Ali, mwanasiasa wa zamani wa Uholanzi ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Uislamu.

Mwaka uliopita, Tucker Carlson, mtangazaji wa chombo cha habari cha Fox News - kinachopendwa na rais Trump, aliwalinganisha bi Hirsi Ali na Ms Omar, akisema: ''Wahamiaji wawili wa Kisomali, mmoja wao anavutia nchini Marekani na mwengine hana ushawishi.."

Huku matukio hayo ya kampeni ya Marekani yakiendelea katika kipindi cha miezi mitano ijayo, unaweza kutarajia matamshi kama hayo kuendelea katika mikutano ya kisiasa ya rais Trump.ku.