Virusi vya corona: Je baridi huchangia maambukizi zaidi ya virusi vya corona?

Watu wengi hawajui iapo vierusi vya corona vinategemea hali ya hewa
Maelezo ya picha,

Watu wengi hawajui iapo vierusi vya corona vinategemea hali ya hewa

Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza jana kwamba msimu wa baridi unaoendelea huenda unachangia pakubwa ongezeko la watu wanaoambukizwa virusi vya corona nchini humo.

Akizungumza baada ya kutangaza idadi mpya ya wagonjwa 544 Waziri Mutahi Kagwe alisema waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini humo baada ya saa 24, waziri Afya Mutahi Kagwe amewataka Wakenya kutokongamana.

Idadi hiyo amesema inajumlisha idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kufikia 19,125.

Wagonjwa hao wapya wanatokana na sampuli 5,259 zilizofanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24.

Maelezo ya picha,

Waziri wa Afya Kenya anasema msimu wa baridi umechangia ongezeko la corona Kenya

Ukweli kuhusu majira ya baridi na joto kuhusu corona ni upi

Kulingana na wataalamu magonjwa mengi ya maambukizi hutokea wakati tofauti katika mwaka.

Flu ama homa hujitokeza katika miezi ya baridi . Magonjwa mengine kama vile Typhus pia hujitokeza wakati wa msimu wa joto.

Kiwango cha ugonjwa wa surua pia hupungua wakati wa msimu wa joto huku maeneo mengine yakiathirika wakati wa kiangazi.

Watu sasa wanakanganyika iwapo virusi vya ugonjwa wa corona Covid-19 ni hatari zaidi.

Tangu kisa cha kwanza kilipotangazwa nchini China katikati ya mwezi Disemba ambao huwa ni msimu wa majira ya baridi , ugonjwa huo kwa kasi huku visa vingi vikiripotiwa katika bara Ulaya na Marekani.

Maelezo ya picha,

Kuna matumaini kwa viwango vya chini vya joto huenda vikapunguza maambukizi ya virusi vya corona

Baadhi ya mataifa ambayo yaliyoathirika zaidi ni yale yenye misimu ya majira ya baridi kali baridi, hatua inayozua uvumi kwamba ugonjwa huo utadhoofika na kuwa hafifu kadri mataifa hayo yanapokaribia miezi ya joto.

Lakini wana ukweli kuhusu hilo kwani virusi vinavyosababisha Covid 19 ni vipya na havina ushahidi kwamba vinaweza kubadilika katika mwaka mmoja.

Hatahivyo Virusi vya Covid-19 , kwa jina Sars, vilisambaa duniani 2003 na vikazuiliwa , ikimaanisha kwamba hakuna data inayojulikana inayoweza kuhusishwa na msimu tofauti kwa mwaka.

Maelezo ya picha,

Utatfiti ulionyesha kwamba Covid 19 huenda nkjali kunapokuwa na joto

Utafiti uliofanywa miaka 10 iliopita na Kate Templeton wa kituo cha magonjwa ya kuambukiza katika chuo kikuu cha Edinburgh , UK ulibaini kwamba aina nyengine tatu ya virusi vya corona vilijitokeza wakati wa baridi na kuendelea kusambaa hadi wakati wa joto.

Virusi hivyo vilionekana kuwa na nguvu kwani vilisambaa kutoka mwezi Disemba hadi mwezi Aprili.

Pia kuna virusi kwa jina Influenza ambavyo pia navyo husababisha virusi vya corona lakini huwaathiri sana wanadamu ambao kinga zao zimedhoofika..

Kuna data chache zinazosema kwamba virusi vya covid 19 vinaweza pia kutofautiana katika mwaka mmoja.

Ukubwa wa mlipuko huu mpya ulimwenguni unaonekana kuwa sawa katika msimu wa baridi na majira ya joto.

Maelezo ya picha,

Kuna tafiti chache ambazo zimebaini mchango wa hali ya anga dhidi ya Covid19

Utafiti ambao haujachapishwa kulinganisha hali ya hewa na maeneo kadhaa ulimwenguni, yaliyofikiwa na Covid-19, unaonyesha uhusiano kati ya kuenea kwa virusi na joto, kasi ya hewa na unyevu.

Utafiti mwingine ambao haujachapishwa pia umeonyesha kuwa joto la juu lilihusishwa na kupungua kwa Covid-19, lakini iligunduliwa katika utafiti huo kwamba hali ya joto pekee haikuweza kuzingatiwa kuwa tofauti ya tukio la ugonjwa huu ulimwenguni.

Wakati huo huo, utafiti mwengine ambao haujachapishwa unatabiri kuwa nchi za wastani na zile zilizopo katika eneo la baridi ziko kwenye hatari kubwa kwa athari za Covid-19.

Nchi ambazo ziko karibu na bahari zimetajwa kuwa ndio zilizoathiriwa kidogo, kulingana na watafiti.

Lakini ukweli, ni kwamba magonjwa ya milipuko hayachangiwi na aina tofauti za hali ya hewa.