Je mashambulio ya Marekani Somalia dhidi ya al-Shabab yana ufanisi wowote?

Somali soldiers
Maelezo ya picha,

Jeshi la Somalia limekuwa likipokea usaidizi wa kijeshi kutoka Marekani

Marekani imefungua ubalozi wake nchini Somalia hivi karibuni baada ya kufungwa kwa miaka 28 kutokanana inachotaja kuwa ni kuimarika kwa usalama sasa ktika taifa hilo la Afrika mashriki ambalo limegubikwa kwa muda mrefu na mzozo.

Tangazo hilo limejiri siku kadhaa baada ya kambi ya jeshi la Marekani kiasi ya kilomita 90 nje ya Mogadishu na ujumbe wa Umoja wa Ulaya kushambuliwa katika mji mkuu na wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu al-Shabab.

Basi je hali imeimarika kweli?

Donald Yamamoto, US ambassador to Somalia
GETTY
"Ni siku muhimu na ya kihistoria inayodhihirisha hatua ilizopiga Somalia katika miaka ya hiviI karibuni."
Donald Yamamoto
Balozi wa Marekani nchini Somalia

Utawala wa rais Trump umeongeza kwa upana misaada na shughuli za kijeshi nchini Somalia tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mnamo 2017, na kufanya kuwa azimio kuu katika jitihada zake duniani kushinda ugaidi wa wenye itikadi kali za kiislamu na kuongeza matumizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani kukabiliana na wanamgambo.

Ongezeko hilo limeandamana na mageuzi katika kugawanywa katika sehemu za taifa la Somalia kwa kutambua "maeneo yanayoshuhudia uhasama", jambo linalomaanisha kuwa makamnda hawahitaji idhini ya kutoka juu kutekeleza mashambulio.

"Makombora hayo ambayo yanahimizwa na kuungwa mkono na serikali kuu Somalia, yanasaidia jitihada za vikosi washirika wetu kuwalinda raia wa Somalia dhidi ya ugaidi ," jeshi la Marekani limeiambia BBC.

Mashambulio ya Marekani Somalia . .  .

Jeshi la Marekani tayari limetekeleza mashambulio zaidi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Hatahivyo ni vigumu kubaini athari ya kweli ya makombora, wataalmu na maafisa wa zamani na wachambuzi katika vyombo vya habari nchini wanaashiria kwamba udhibiti wa kundi hilo katika maeneo waliomo bado ni mzito.

Kuna wasiwasi pia kuwa raia wanajikuta katikati ya mzozo huo.

Amnesty International - shirika la kimataifa la kutetea haki za binaaamu limechapisha matokeo kuwa mashambulio hayo yamesababisha mauaji ya watu wasiokuwa wafuasi wa makundi yoyote ya wanamgambo licha ya kwamba Marekani inasisitiza kuwa inawalenga wanamgambo wa al shabab pekee.

Wachambuzi wanasema mashirika ya kijamii, ambayo katika siku za nyuma yaliuga mkono makombora hayo , yamechoshwa kwa msururu wa mashambulio hayo yanayotekelezwa sasa.

Kwahivyo ongezeko la mashambulio ya Marekani limesaidia?

Bado Al-Shabab linaendelea kudhibiti sehemu kubwa za mahsindani za Somalia na linaendelea kuidhinisha mashambulio katika maeneo ya mijini.

Mashambulio mengi yametokea mjini Mogadishu na eneo la Lower Shabelle karibu na mji mkuu huo.

Kumeshuhudiwa mashambulio machache katika eneo la kaskazini mwa nchi licha ya kwamba kuna makundi yanayolitii kundi la Islamic State katika eneo la kaskazini mashariki.

Katika miaka ya hivi karibuni, kundi hilo limebadili mbinu kutoka kukabiliana moja kwa moja na jeshi na kugeukia mbinu za kuzusha ghasia, kama milipuko, uvamizi na mauaji ya wasomali na maafisa wa kimataifa.

Limeendelea kufanikiwa pia kukusanya mapato kutoka koo mbalimbali, kwa kukusanya ushuru na kuendesha mahakama nje ya maeneo yanayodhibitiwa na serikali.

"Al-Shabab limeondolewa kwa ukubwa kutoka maenoe yenye watu wengi lakini ushawishi wake mijini huenda unaongezeka kwa mara nyingine," anasema Michael Keating, aliyekuwa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Somalia (UNSom) kuanzia 2016 hadi 2018.

Serikali ya Somalia haichapishi takwimu kuhusu mauaji ya wanamgambo.

Hatahivyo, mradi wa the Armed Conflict Location & Event Data Project (Acled) unakusanya data za mashambulio ya al-Shabab kwa kutumia duru za ndani ya nchi nza za kimaaifa.

Mashambulio ya Al-Shabab nchini Somalia. Idadi ya vifo kwa mwaka.  Mnamo 2017, zaidi ya watu  500 waliuawa katika shambulio moja la kigaidi. Takwimu za 2019 ndio zilizopo hivi sasa na zinajumuisha vifo vya wanajeshi na raia. .

Hii inaashiria kuwa mwaka huu 2019 tayari ni mwaka ulionakili idadi kubwa ya vifo kutokana na mashambulio ya al-Shabab.

Idadi hii ipo chini kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na iliokuwepo katika mwaka mzima wa 2017 ambapo watu 500 waliuawa katika shambulio moja mjini Mogadishu lililohusisha mabomu katika malori mawili.

Serikali ilitaja al-Shabab, kuhusika na shambulio hilo licha ya kwamba kundi hilo halikukiri binfasi kuhusuika.

Wataalmu maalum wanaofuatilia shughuli za kijihadi wanakadiria idai ya wanamgambo wa al Shabab katika eneo kuwa baina ya 5,000-7,000.

"Huwezi kurusha mabomu kutafuta amani Somalia. Iwapo ghasi zitapunguzwa kunahitajika wazi kuwepo mfumo wa kisiasa unaoruhusu watu kuzungumza badala ya kufyetua risasi na kutekeleza mauaji," anasema Keating.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje Marekani ameiambia BBC kuwa taifa hilo limesalia kuwa mfadhili mkuu wa kimataifa kwa Somalia na inawajibika kuleta utulivu kwa nchi hiyo.