Bibi harusi wa kihindi aliyevalia suti

Sanjana Rishi and Dhruv Mahajan at their wedding

Sanjana Rishi anasema hivi karibuni aliamua kuvalia suti katika harusi yake badala ya mavazi ya kitamaduni ya bibi harusi wa kihindi kwasababu "anapenda suti".

Lakini katokana na chaguo la vazi la siku ya harusi yake, pia aliwasilisha ujumbe mkubwa katika ulimwengu wa mitindo - ambao umewaacha baadhi ya watu wakitafakari ikiwa wakati umewadia kwa mabibi harusi kuachana na kasumba ya kitamaduni na kuvalia suti.

Katika nchi za magharibi, mtindo wa mabibi harusi kuvalia suti umepata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.

Wanamitindo wamekuwa wakijumuisha suruali ndefu katika mavazi mkusanyiko wa nguo za harusi na zimeungwa mono na wasanii maarufu

Mwaka jana, muigizaji wa filamu ya 'Game of Thrones' Sophie Turner alivalia suruali ndefu nyeupe alipofunga ndoa na mwanamuziki Joe Jonas mjini Las Vegas.

Lakini, mavazi ya Bi Rishi hayakuwa ya kawaida India- ambako bibi harusi huvalia sari (sketi ndefu, blauzi- na mtandio). Rangi inayopendelewa zaidi ni nyekundu iliyo na marembo ya dhahabu au fedha.

"Sijawahi kuona Bibi harusi wa Kihindi aliyevalia namna hii," anasema Nupur Mehta Puri, mhariri wa zamani wa jarida la mabibi harusi.

"Mabibi harusi huwa wanapenda kuvalia mavazi ya kihindi na bangle za kutamaduni wanazopewa na mama au mabibi zao.

"Wiki kilikuwa kitu kipya kabisa.Na alivutia sana."

Bi Rishi, 29, Mfanyabiashara wa India aliye na uraia wa Marekani, aliooana na mfanyabiashara wa Delhi Dhruv Mahajan, 33, tarehe 20 Septemba katika mji mkuu wa, Delhi.

Aliwahi kufanya kazi ya uwakili nchini Marekani kabala ya kurejea India mwaka jana na wapenzi hao wamekuwa wakiishi pamoja kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Walikuwa wamepanga kufanya harusi yao mwezi Septemba nchini Marekani- ambako ndugu yake bibi harusi na baadhi ya marafiki wake wanaishi - na harusi ya pili ambayo ingelikuwa ya utamaduni wa kihindi ifanyike mjini Delhi mwezi Novemba.

Lakini jana la Covid lilipotokea mipango yao ''ikasambaratika kabisa''.

Tofauti na Marekani, uhusiano wa wachumba kuishi pamoja kabla ya kuoana rasmi hairuhusiwi nchini India.

Bi Rishi anasema japo wazazi wake "walikuwa hawana tatizo na uamuzi wa mimi na mchumba wangu kuishi pamoja kabla ya kuoana, kulikuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jamaa na marafiki kuwataka wafanye rasmi uhusiano wetu. Kwa hivyo mwisho wa mwezi Augosti, "Asubuhi moja niliamka na kuamua , 'wacha tuoane'".

Bi Rishi anasema alipoamua kuolewa alijua anataka muonekana wa aina gani na atavalia nini.

"Nilijua nitavalia suti na nilijua ni suti aina gani," alisema.

Alipokuwa akifanya kazi ya uwakili nchini Marekani, alipendelea sana kuvalia sana suti kwani "mwanamke wa kisasa niliyemhisudu" alivalia hivyo pia.

"Nimekuwa nikivutiwa sana na mwenendo wa wanawake wanaovalia suti. Hali iliyonifanya kuvutiwa na vazi hilo na kulivalia muda lote."

Pia magazine hayo yalikaa saga kwasababu waliyokuwepo ni jamaa wa karibu wa familia pekee, yani kulikuwana watu 11 ukijumuisha bwana na Bibi harusi na mchungaji.

"Waliohudhuria walilikuwa wazazi wetu na babu na bibi zetu. Harusi ilifanyika nyumbani kwa kina Dhruv. Kila mmoja alikuwa amevalia mavazi yakawaida tu, ningelikuwa tofauti sana laiti ningelivalia mavazi halisi ya harusi."

Bwana Mahajan anasema hakutarajia mchumba wake atavalia suti.

"Hadi nilipomuona, sikujua atavalia nini, lakini sikuwa na wasiwasi kwasababu nilijua Sanj anapendeza akiwa na magazine ya aina yoyote."

Anakiri kuwa, alipomuona mara ya kwanza hakujua amevalia suti ya suruali, "Alipendeza sana".

"Naweza kuendelea kusifia uzuri," alisema huku akicheka kwa furaha.

Nguo ya harusi ya Bi Rishi ilisababisha gumzo mtandaoni.

Baada ya kuweka picha ya muonekano wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, marafiki walimpongeza sana ana kusifia nguo yake baadhi yao wakimpatia jina la "Bibi harusi wa kisasa".

Wanamitindo wamavazi Pia walimpongeza kwa kuchagua vazi hilo la kipekee

"Jamani, umependeza sana!!!" aliandika mwanamitindo Masaba Gupta; na mzalishaji wa filamu ya kihindi ya Rhea Kapoor alisema. Nae ndada yake mwigizaji Sonam Kapoor, alitaja vazi hilo kuwa "zuri sana".

Anand Bhushan, mimosa wa mwanamitindo tajika wa mavazi ya wanawake, aliambia BBC jinsi alivyopendezwa na suti ya Bi Rishi na kuongeza kuwa "ni muonekano mzuri wa bibi harusi".

"Nilipoona picha zake, mara ya kwanza kilichonijia mawazoni ni kwamba, '' Carrie Bradshaw [mmoja wa waigizaji wa sinema ya Sex and the City] angelikuwa mhindi angellivalia hivi wakatiwa harusi yake."

Lakini baadhi ya watu wanaofanya biashara ya nguo za mabibi harusi walipoanza kusambaza picha zake, alianza kukosolewa vikali na wale ambao hawakupendelea.

Katika ujumbe walisema ameaibisha jamii na utamaduni wake, na kumuonya mama wake kuwa ameoana na mtu ambaye anatafuta sifa na ambaye yuko tayari kufanya lolote kwa jina la kupigania haki za wanawake.

Baadi yao walisema hawezi kuelewa utamaduni wa kihindi kwasababu mawazo yake yametekwa na utamaduni wa magharibi. Wengine "waliniambia niende nikajiue".

Bi Rishi anasema haelewi wanaomkosoa kwa samabu "Wanaume wa kihindi huvalia suruale ndefu wakati wa harusi na hakuna anayewakisoa - lakini mwanamke anapofanya hivyo kila mmoja anamjadili".

"Lakini nadhani ni kwasababu wanawake wanatakiwa kufikia viwango vya juu zaaidi vya maadili katika jamii," anasema.

Sio nchini India pekee ambako wanawake wanapigania haki ya kivaa suruali ndefu. Jitihada hizo zimekuwa zikiangaziwa kote duniani huku tamaduni nyingi hata katika jamii ya kisasa ikimhukumu mwanamke anayejaribu kuachana na vazi la nguo za jadi kwa wanawake.

Hadi mwaka 2013, ilikuwa hatia kwa wanawake kuvaa suruali ndefu nchini Ufaransa japo marufuku hiyo imepuuziliwa mbali kwa miongo kadhaa.

Nchini Korea Kusini, wanafunzi wa kike waliruhusiwa hivi karibuni kuunua suruali badala ya sketi ambayo ilikuwa sehemu ya sare zao.

Mwanafunzi wa kike huko North Carolina Marekani alilazimika kwenda kotinin ili aruhusiwe kuvaa suruale shuleni hata wakati wa msimu wa baridi kali.

Katika jimbo la Pennsylvania, msichana wa miaka 18 alikabiliana kisheria na shule yake kupata haki ya kuruhusiwa kuvaa suruale ndefu mwaka jana na kushinda.

Visa vya wanawake kuzuiliwa kuvaa suruali vinaendelea kushuhudiwa nchini India.

"Japo wanawake wa India wamekuwa wakivalia aina fulani ya suruali ya kushonwa au pyjama kwa karne kadhaa, nje ya miji mikuu familia za kihafidhina haziwaruhusu wanawake kuvalia suruali ya kawaida au jeans," Bwana Bhushan anasema.

"Katika Jamie ilijawa na taasubi ya kiume, wanaume wamekuwa na hofu kuhusu wanawake kujifanyia maamuzi, kwa hivyo wanataka kuwaamulia karibu kila kitu, uhuru wao wa uzazi, jinsi wanavyozungumza na kucheka aua hata mavazi yao," anaongeza .

Japo Bi. Rishi anasema alipoamua kuvalia suti hakuwa anajaribu kuwasilisha ujumbe wa kisiasa, ameafiki kuwa wakati mmoja ataingia ulingoni.

"Niligundua kuwa sio wanawake, hasa nchini India wako huru kuvalia mavazi wanayopenda. Picha zangu ziliposambaa kwenye Instagram baadhi ya wanawake waliandika ujumbe wakisema kwamba angalau wamepata ujasiri wa kutofautiana na wazazi wao au wake lao kuhusu mind wa magazine wangelipendelea kuvaa wakati wa harusi zao

"Kwa kweli nilifurahi sana kusikia hilo lakini kwa upande niliingiwa na hofu huenda nikavuruga maisha ya watu wenginena kuleta shida majumbani mwao.'"

Lakini swali ni je bibi harusi huyu aliyeamua kuvalia suti anaweza kuwashawishi wengine kufanya hivyo?

Mavazi yake ambayo sio ya kawaida huenda ''yamezua gumzo - ambalo linaweza kuendelea au kufifia," Bwana Bhushan anasema

"Natumai hilo litawezekana siku zijazo."