Pakistan yaitaka Facebook kupiga marufuku maudhui ya chuki dhidi ya Uislamu

Pakistan Prime Minister Imran Khan makes a brief statement to reporters before a meeting with U.S. House Speaker Nancy Pelosi
Maelezo ya picha,

Imran Khan amekata ujumbe wa chuki zifutwe Facebook

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amemuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg, akimuomba aweke marufuku ya maudhui ya chuki dhidi ya uislamu.

Katika barua hiyo, Bwana Khan amesema "kuongezeka kwa chuki dhidi ya uislamu" kunachocha "chuki, itikadi kali na ghasia….hasa kupitia matumizi ya mitandao ya habari ya kijamii ".

Hii inakuja baada ya Bwana Khan kumshutumu rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa "kuushambulia Uislamu".

Tayari Facebook ina sera ya kuondoa kauli za chuki kwenye majukwaa yake.

Inaelezea kauli ya chuki kama ''shambulio la moja kwa moja dhidi ya watu'' kwa misingi ya jamii, kabila, taifa asili na imani ya watu kupitia "kauli za ghasia au zinazodhalilisha " au "ubaguzi wenye madhara ".

Katika barua hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, Bwana Mr Khan alitoa mfano wa uamuazi wa hivi katribuni wa Facebook wa kuzuwia maudhui yoyote ambayo yanakataa au kupotosha ukweli kuhusu Holocaust.

Alitoa wito wa sera sawa na hiyo iwekwe kuhusiana na kauli dhidi ya Uislamu.

"Kutokana na kuongezeka kwa ukiukaji na udhalilishaji wa Waislamu katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, ningeomba uweke marufuku dhidi ya kauli za Chuki dhidi ya Uislamu na chuki za Uislamu katika Facebook sawa na ile uliyoweka kwa ajili ya Holocaust," alisema.

"Ujumbe wa chuki lazima upigwe marufuku kwa ujumla-mtu hawezi kutuma ujumbe huku ujumbe dhidi ya baadhi haukubaliki, huu unakubalika dhidi yawengine ."

Jumapili, Bwn Khan alimshutumu rais wa Ufaransa "kuushambulia Uislamu ".

Maelezo ya picha,

Mwalimu aliyechinjwa baada ya kuwaonesha wanafunzi wake vibonzo vya Mtume Muhammad darasani.

Kauli zake zimekuja baada ya Bwana Macron kutoa hotuba yake kumuhusu Mwalimu Mfaransa wa somo la Historia ambaye aliuawa baada ya kuwaonesha wanafunzi wake vibonzo vya Mtume Muhammad darasani.

Bwana Macron alisema kuwa mwalimu "aliuawa kwasbabu Waisalmu wanataka maisha yetu yajayo ",lakini Ufaransa haita "acha katuni zetu".

Katika ujumbe wake wa Twitter, Bwana Khan alijibu : "Inasikitisha kwamba Bw Macron amechagua kuendeleza chuki dhidi ya Uislamu badala ya magaidi wanaofanya ghasia "

Bwana Khan, ambaye kwa sasa anakabiliwa na shinikizo kutoka muungano wa vyama vya upinzani , amekuwa akifahamika kwa kutumia dini kuimarisha ngome yake.

Wito watolewa wa kususia bidhaa za Ufaransa katika nchi za Kiarabu

Wito watolewa wa kususia bidhaa za Ufaransa katika nchi za KiarabuImage caption: Wito watolewa wa kususia bidhaa za Ufaransa katika nchi za Kiarabu

Kampuni kadhaa za Uarabuni zimeondoa bidhaa zake Ufaransa kutokana na kauli ya rais Emmanuel Macron dhidi ya vibonzo vya Mtume Muhammad.

Rais Macron alisema Ufaransa haitoacha kuchora vibonzo, kutokana na kuchinjwa kwa mwalimu Samuel Paty aliyewaonesha wanafunzi wake kibonzo cha Mtume Muhammad mapema mwezi huu, katika kitongoji kimoja cha Paris katika somo kuhusu uhuru wa kujieleza.

Siku ya Ijumaa vibonzo vya Mtume Muhammad vilichapishwa kwenye majengo ya serikali nchini Ufaransa, hatua iliyokasirisha nchi za Kiarabu.

Wito wa kususia bidhaa za Ufaransa unavuma kwenye mitandao ya kijamii, huku wananchi wa Misri wakisambaza orodha ya bidhaa za Kifaransa walizoamua kuzisusia.