Uchaguzi Tanzania 2020: Kwanini wanamuziki nyota Tanzania wamuunga mkono Rais Magufuli?

uchaguzi
Maelezo ya picha,

Rais Magufuli alikuwa akiwapongeza wanamuziki kwa kuwavesha kofia yake

Katika mikutano ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) , maneno ya nyimbo za hivi karibuni yamekuwa yakibadilishwa kumsifu Rais John Magufuli, ambaye anawania muhula wa tatu madarakani katika uchaguzi utakaofanyika Jumatano wiki hii.

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ameuchanganya upya wimbo wake maarufu kwa jina Baba Lao - kuwa "Magufuli Baba Lao".

Wimbo huo haumsifu Rais Magufuli pekee, bali pia Makamu wa rais Samia Suluhu, Waziri mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine pia wa CCM.

Upinzani pia una wanamuziki katika kampeni zake, japo sio wengi.

Mbinu hii ya kutumia wanamuziki katika kampeni - kuwavutia wapigakura vijana -haishangazi kutokana na kwamba theluthi mbili ya idadi ya Watanzania ni vijana wenye chini ya umri wa miaka 25.

Kihistoria pia, si jambo lisilo la kawaida kwa wanamuziki kutunga nyimbo za kisiasa, anasema Dkt Viscencia Shule, mhadhiri na mtaalamu wa sanaa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

"Wasanii na wanamuziki wamekuwa wakihusika katika mapambano ya uhuru nchini Tanzania na ikaendelea hivyo baada ya uhuru. Wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa ."

'Uaminifu ni muhimu'

Lakini Dkt Shule haamini kuwa nyimbo zote za kusifu ni halisi.

Hii hasa ni kwasababu ya sheria kali zilizoanzishwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ili kuwadhibiti wanamuziki na rais anayedai uaminifu.

Mwezi Julai, Rais Magufuli aliwaita mahasimu wawili wa muda mrefu - Diamond Platnumz na Alikiba -kushiriki mkutano wa kampeni katika mji Dodoma, ambako aliwafanya wanamuziki hao kuzika tofauti zao.

Maelezo ya sauti,

Kuna athari gani kwa wanamuziki kujihusisha na kampeni za kisiasa?

Mwanamuziki mwingine nyota, Harmonize,pia alikuja -ingawa pia alikuwa amekosana na Diamond Platnumz baada ya kujiondoa katika nembo ya Wasafi .

"Nanijihisi vizuri ninapomuona Alikiba akiwa ameketi kando ya Diamond. Unapomuona Harmonize, ambaye alimuacha Diamond, akimsifu hadharani, huo ndio umoja ninaotaka ," rais alinukuliwa akisema

'Kuoneshana ubabe'

Lakini Diamond Platnumz hajawa na uhusiano mzuri wakati wote na mamlaka- na katika kipindi cha miaka michache iliyopita alilazimika kuwaomba msamaha mara kadhaa.

Mwaka 2018 alikabiliwa na mtihani mkbwa wakati alipokiuka sheria kali ikiwemo " ukiukaji wa maadili ya muziki ''-kulingana na waziri mmoja.

Sheria hizo zimekuwepo kwa miaka, lakini sasa zinatekelezwa kikamilifu na baraza la Sanaa Tanzania Basata, ambalo mara kwa mara limekuwa likipiga marufuku nyimbo zinazoangaliwa kuwa zinakiuka maadili na za matusi.

Mwezi Aprili 2018 Diamond Platnumz alihojiwa na polisi baada ya kuweka kwenye mtandao wa Instagram video yake akimbusu mwanamke.

Miezi minane baadaye alipigwa marufuku kufanya shoo nchini Tanzania baada ya kucheza wimbo ambao Basata ilisema unamaudhui ya kingono.

Lakini hatimaye alijishusha chini na kuiomba mshamaha Basata kupitia mitandao ya kijamii Disemba mwaka 2018.

'Suala la kuogopa'

Maelezo ya picha,

Roma Mkatoliki akizungumza na vyombo vya habari

Kupitia Basata wanamuziki wamekuwa wakichunguzwa na kuidhibitiwa na wamelazimika kujifunza kwa miaka mitano kwamba lazima wawe makini na kazi yao.

Hata mwezi Septemba kituo cha radio ya Diamond Platnumz kilizimwakwa wiki kwa kutangaza kipindi kilichokuwa na baadhi ya maudhui ya ukiukaji wa maadili.

"Baadhi ya hali zinaweza kuwasukuma kuimba sifa ili kunusuru maslahi yao ,"anasema Dkt Shule .

Baadhi ya wanamuziki, mara kwa mara wenye uhuru na familia kubwa,huishi katika hali ya umasikini.

"Baadhi wanafurahia kufanya hivyo, ili kuonekana tu … Lakini kuna jambo kuu zaidi - uoga ," aliongeza.

Baadhi wanaweza kuamini kuwa wanaweza kupata upendeleo fulani kutoka kwa Rais Magufuli, zikiwemo nyadhifa fulani za kitaifa.

Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale, ambaye alianzisha naye nembo ya muziki ya WCB , alishiriki kinyang'anyiro cha kuwania ubunge kupitia CCM na hana wapinzani katika jimbo lake.

Kuna wasanii wengine ambao wanawania nyadhifa za kisiasa katika uchaguzi, wengi wao wakigombea kupitia tiketi ya chama tawala cha CCM , ikiwa ni pamoja na mwanamuziki wa rap Mwana FA.

Maelezo ya sauti,

Mwana FA na Wakazi: Wanamuziki wa tanzania waelezea sababu zao za kujitosa katika siasa

Wasanii wanalazimika kuimba kwa sababu mbalimbali ," anasema Dkt Shule.

"Wengi wao bila shaka hawataki kufanya hivyo . Lakini kama wasipokiimba chama tawala , wanaonekana wanauunga mkono upinzani.

"Nakama wanapinga watapata athari zake…upinzani umeumia sana ,"anasema msomi huyo.

Mfano ni mwanamuziki wa mzuki wa rap Roma Mkatoliki, maarufu kwa nyimbo zake za kuipinga serikali, anayesema alitekwa nyarana watu wane wasiojulikana mwezi Aprili 2017, akateswa na baadaye kutupwa karibu na bahari mjini Dar es Salaam siku tatu baadae.

Mahasimu katika uchaguzi wa Tanzania:

Mwaka jana alihojiwa kwa wimbo wake ulioikosoa serikali, ambao vituo vya redio viliamua kutoucheza .

Mwanamuziki wa rap Nay wa Mitego pia alikamatwa mwak 2017 kwa wimbo ambao alijumuisha mstari uliosema'' kwani bado kuna uhuru wa kujieleza nchini?"

Alionekana kuwa alikataa kutishwa, na yuko katika kampeni za chama cha upinzani za chama cha Chadema.

Lakini hakuna wimbo wake uliopigwa marufuku kwa miaka mitatu-na anaonekana kuficha ukosoaji wowote kwa namna ambayo inaweza kuwa vigumu kumuwajibisha kwa kile hasa alichokimaanisha.

Katika wimbo wake wa hivi karibuni, ''Mungu Yuko Wapi?'' alihoji uwepo wa Mungu na imani yake, akimuuliza Mungu ni kwanini anaruhusu madikteta kuwepo na kujifanya kama miungu.