Cristiano Ronaldo apata virusi vya corona

Ronaldo alicheza mechi Jumapili
Maelezo ya picha,

Ronaldo alicheza mechi Jumapili

Cristiano Ronaldo: Mchezaji wa Ureno na Juventus apata virusi vya corona, shirikisho la soka la Ureno,Portuguese Football Federation (FPF) limetangaza.

Mchezaji huyo mwenye miaka 35-anaendelea vizuri bila ya kuwa na dalili zinazoonyesha corona na amejitenga na watu kwa sasa", taariofa kutoka FPF imesema.

Ureno inatarajia kucheza na Sweden katika ligi la kitaifa hapo kesho Jumatano.

Mchezaji mwingine wa kikosi cha Ureno Fernando Santos amekutwa na corona pia na miongoni mwa ambao watakuepo kwenye mechi ya Jumatano.

Ureno ilitoka sare 0-0 dhidi ya Ufaransa ,mjini Paris Siku ya Jumapili na wanaongoza kundi wakiwa na alama sawa dhidi ya Ufarasa ambao ni mabingwa wa dunia.

Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza barani ulaya kufunga magoli 100 katika ngazi ya timu ya taifa.

Nyota huyo aliweka selfie yake akiwa na kikosi cha Portugal katika mtandao wa kijamii Jumatatu usiku na kuandika ''Umoja ndani na nje ya uwanja''

Kutokana na muda atakaokaa kwenye karantini, Ronaldo pia atakosa mechi ya Juventus Oktoba 17 na mechi ya ufungu ya Champions League awamu ya makundi dhidi ya Dynamo Kiev Oktoba 20.